Kisa refa kupigwa, Rais asimamisha Ligi
Eric Buyanza
December 12, 2023
Share :
Shirikisho la soka nchini Uturuki kupitia kwa Rais wa Shirikisho hilo Mehmet Buyukeksi limetangaza kusimamisha michezo yote ya Ligi zote kufuatia shambulio la muamuzi Halil Umut Meller.
Muamuzi Halil Umut Meller alishambuliwa kwa kupigwa ngumi na Rais wa Klabu ya Ankagarucu Mr Faruk Koca kutokana na timu yake kuruhusu goli la kusawazisha 1-1 dhidi ya Rizespor dakika ya 97 ya mchezo huo wa Ligi Kuu Uturuki.