Kisa show ya Diamond Baba Levo alia na Taifa Stars.
Joyce Shedrack
December 29, 2025
Share :
Baba Levo ambae ni Mbunge wa Kigoma Mjini baada ya show ya Mwanamuziki Diamond Platnumz huko Nchini Benin yeye ametoa mtazamo wake akilinganisha show ile na timu ya Taifa, Taifa stars akidai kuwa spirit ya upambanaji na kujituma ya Diamond katika kuliwakilisha Taifa inatakiwa itumike pia kwa Wachezaji wa Taifa stars ili kuleta Matokeo chanya kwenye Mpira wa Tanzania.
Ujumbe huu kutoka Kwa Mh. Clayton Revocatus #BabaLevo unatokana na matokeo yasiyoridhisha baada ya Taifa stars kupata sare kwenye mchezo wake dhidi ya Uganda huku akifungwa na Nigeria na kubakisha Mchezo Mmoja dhidi ya Tunisia wakiwa na alama moja pekee katika Michuano ya AFCON 2025 huko Morocco.
"TAREHE 28/12/2026 LUKUGA #BENIN HUU NDIO UWAKILISHI WA TAIFA SASA..!!
NA KAMA TAIFA STARS WANGEKUWA WANAJITUMA KAMA LUKUGA @diamondplatnumz BASI TUNGEPATA MATOKEO CHANYA SANA KWENYE MPIRA WETU…!!!
#Lakini Hii Tabia Ya Kila Mtu Akikamata Mpira Anawaza Back Pass Au Anawaza Anao Anao Mpaka Anyang’anywe Itakuwa Ni Safari Ya Utalii Moroco📌" Ameandika Baba Levo.





