Kisa soksi mechi ya Arsenal na Chelsea yaahirishwa nusu saa
Sisti Herman
March 17, 2024
Share :
Mechi ya ligi kuu wanawake nchini Uingereza Kati ya klabu ya Arsenal na Chelsea imelazimika kuchelewa kwa karibu dakika 30 kwasababu timu zote mbili zilivaa soksi zinazofanana jambo ambalo ni kinyume na kanuni.
Timu hizo ziliingia uwanjani kupasha misuli moto zote zikiwa zimevaa soksi nyeupe baada ya mwamuzi kuingilia kati ililazimika Arsenal kununua soksi za rangi tofauti kwenye duka la Chelsea.
Arsenal walilazimika kuficha kwa gundi nembo za Chelsea na mtengenezaji wa vifaa kampuni ya Nike kwasababu za kiushindani na kibiashara.
Mchezo huo ulitamatika kwa Chelsea kushinda 3-1.