Kisa unyanyasi wa ngono, Melo awakataa Alves na Robinho
Sisti Herman
March 28, 2024
Share :
Kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa ngono zinazowakabili marafiki zake Dani Alves na Robinho ambayo wamefanya kwa nyakati tofauti, mchezaji mkongwe wa Brazil ambaye aliwahi kucheza Inter Milan, Juventus na timu ya Taifa ya Brazil ambaye kwasasa anacheza klabu ya Fluminense ya Brazil Felipe Melo amesema mastaa hao wa zamani wa Real Madrid na Barcelona wanapaswa kuvuna walichopanda.
"Mimi nina binti wa miaka 15, kama wangemfanyia hivyo binti yangu tusingekuwa tumekaa hapa, wanapaswa kulipa kulingana na waliyoyafanya" alisema Felipe Melo.