Kisa ushirikina, Kibu na Mzamiru wafungiwa
Sisti Herman
March 14, 2024
Share :
Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi kuu Tanzania bara kwenye ripoti yake ya kikao kilichoketi juzi machi 12 iliyotolewa leo machi 14 imetoa adhabu kwa vilabu na wachezaji mbalimbali kwa kukiuka kanuni za uendeshaji na usimamizi wa ligi huku wachezaji wa klabu ya Simba Kibu Denis na Mzamiru Yassin wakikumbawa na rungu la faini.
Wachezaji was Simba, Kibu Denis na Mzamiru Yassin wametozwa faini ya Sh. 1,000,000 kila mmoja kwa kosa la kuondoa taulo la mlinda mango wa Coastal Union litilokuwa limewekwa pembeni ya lango wakati mchezo ukiendelea, jambo lililoashiria imani za kishirikina.