pmbet

Kisiwa ghali zaidi kulala Afrika kipo Tanzania, Milioni 100 kwa usiku mmoja

Sisti Herman

May 27, 2026
Share :

 

Kisiwa kidogo cha Thanda kilichopo Mafia, mkoa wa Pwani kimeripotiwa kuwa ndiyo kisiwa ghali zaidi kwa mtu kwenda kupumzika kwa usiku mmoja kwani kinagharimu hadi Dola za kimarekani 40,750 (zaidi ya Tsh Mil. 106).

Kukodi kisiwa hicho ni kuanzia siku 5 ambapo itakugharimu kulipia zaidi ya Tsh Mil. 500 Mil. na unapokodi haukodi chumba tu, bali unakodi kisiwa kizima kwaajili yako na watu wako (watu 10 hadi 28 kulingana na mpangilio).

Gharama hizo zinajumuisha timu nzima ya wafanyajkazi wa kisiwa watakaokuwa wanawahudumia wakiwemo wapishi binafsi, wahudumu na manahodha wa boti. vYakula na vinywaji vya bei ghali na huduma za Spa zimejumuishwa pia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet