pmbet

Kispika cha Ahmed Ally kutamba Durban Afrika Kusini.

Joyce Shedrack

April 24, 2025
Share :

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally ametangaza siku ya leo kuwa watafanya hamasa katika Jiji la Durban Nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Stellenbosch katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Saleh Jembe – Page 271 – Official Website

Akizungumza kupitia Simba TV ikiwa ni siku ya pili wakiwa Nchini humo kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi wa Nusu Fainali katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika ngazi ya klabu Ahmed Ally amesema watapita kwenye mitaa ya Durban kwenda kuzungumza na Wanansimba.

 

'Tunachotaka ni kuwatia unyonge wapinzani wetu hapa hawana watu hata kidogo kitakachowabeba ni u South Africa tu lakini hawana mashabiki hapa Durban tunataka kuwatia unyonge nyumbani kwao yaani wanashuka pale Moses Mabhida wanakuta uwanja umetawala nyekundu na tumekuja na Mabendera makubwa" Amesema Ahmed Ally. 

 

Ahmed Ally hajaweka wazi ni siku gani ataanza hamasa hiyo lakini amesema siku ya kesho ndiyo siku ambayo mashabiki wengi watawasili Afrika Kusini kutokea nyumbani Tanzania.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet