Kitasa cha Morocco kuwanoa AS Vita
Sisti Herman
January 12, 2024
Share :
Klabu ya AS Vita ya DR Congo imemtambulisha beki wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco na klabu ya Fulham ya ligi kuu Uingereza Abdeslam Ouaddou kuwa kocha wao mkuu.
Kitasa hicho cha zamani chenye umri wa miaka 45 sasa atakabiliwa na mtihani wa kurudisha AS Vita kuwa timu tishio kwenye mashindano ya ndani ikiwemo League 1 na michuano ya Afrika kama ilivyokuwa miaka iliyopita.