Kitenge atambulishwa rasmi PM-Bet
Sisti Herman
January 24, 2024
Share :
Mtangazaji mashuhuri wa vipindi vya michezo nchini Maulid Kitenge ametambulishwa rasmi kuwa balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Playmaster Gaming Coorperation limited (PM-BET) ambayo inatambuliwa rasmi na bodi ya michezo ya kubahatisha (Gaming Board of Tanzania).
“Imekuwa siku ya kipekee kumpata Kitenge, najua wana PM-Bet wapo wengi sana Tanzania na najua kupitia Kitenge wataona zaidi kwasababu watu wengi wanamfuatilia, watu wengi wanamsikiliza” alisema William Kimonge, Operation Manager wa PM Bet
"Kiukweli kampeni kama ya Royal Sports ni kubwa watu wanashinda magari ya kifahari, pikipiki na fedha hivyo inahitjai mtu mzito kidogo kuitangaza" alisema Kitenge mara baada ya Kutambulishwa kwake
Kitenge anakuwa mtu maarufu zaidi mwingine kuitangaza PM Bet mara baada ya mrembo Hamisa Mobetto na msanii Rayvanny kuitangaza kampuni hiyo kwa nyakatio tofauti.