Kituo chafanyia wateja wake 'Massage' kwa kutumia nyoka
Eric Buyanza
March 4, 2024
Share :
Kituo kimoja cha kufanyia masaji (massage) huko mjini Cairo Misri, kinatumia nyoka walio hai kufanyia wateja wake masaji ya mwili.
Mmiliki wa kituo hicho Safwan Sedki anasema hutumia mchanganyiko wa aina 28 tofauti za nyoka wasio na sumu katika masaji ya mtu mmoja ambayo huchukua takriban dakika 30.
Kwa mujibu wa Safwan, masaji ya nyoka imethibitishwa kupunguza maumivu ya misuli na viungo huku ikiweka sawa mzunguko wa damu. (Reuters)