pmbet

Kiungo aelezea Bocco alivyomsaidia kabla kisaikolojia

Sisti Herman

January 2, 2024
Share :

Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba Salehe Karabaka amefunguka namna alivyopewa motisha na nahodha mkuu wa timu hiyo John Bocco na kocha mkuu wa timu hiyo Abdelhack Benchikha na kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa timu hiyo ndani sekunde chache baada ya kupata nafasi.

 

“Wakati nipo  nje nikijiandaa kuingia, kocha na nahodha kuna kitu waliniambia, nahodha aliniambia ukipata nafasi usiwe na presha, cheza onyesha kama kawaida kwahiyo nilivyoingia nikafuata na maelekezo ya kocha, kocha aliniambia tukiwa tuna mpira nicheze pembeni kwenye chaki, niibie pembeni ili mtu mwenye mpira aweze kuniona na kunipa, ndivyo nilivyofanya” alieleza Karabaka kwenye mahojiano idara ya habari ya Simba.

 

“Ngoma (Fabrice) aliniambia lazima nifunge kwasababu nacheza na timu yangu ya zamani hivyo nawajua zaidi, ndiyo maana nilivyofunga tu alionekana kushangilia sana na kunipiga vibao vingi” alimaliza Karabaka

 

Karabaka amefanya hivyo masaa machache baada ya kutambulishwana kusajiliwa kwake kutoka JKU ya Zanzibar.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet