Kiungo bora wa Italia kumrithi Kevin De Bruyne Man City.
Joyce Shedrack
June 4, 2025
Share :
Klabu ya Manchester City imefikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Timu ya Taifa ya Uholanzi na klabu ya AC Milan Tijani Reijnders mwenye umri wa miaka 26 ili kurithi nafasi ya Kevin De Bruyne ambaye hatakuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao.
Man City imeanza mazungumzo rasmi na AC Milan ili kunasa saini ya nyota huyo mapema ambaye alikuwa na kiwango bora msimu uliomalizika katika ligi ya Italia Serie A na kuchaguliwa kuwa kiungo bora wa msimu wa ulioisha.
Nyota huyo bado anamkataba wa AC Milan unaotarajia kutamatika June 30 mwaka 2030.