Kivumbi leo..! ni vita ya Harry Kane na Guirassy Der Klassiker.
Joyce Shedrack
November 30, 2024
Share :
Dabi namba moja kwa ukubwa Nchini Ujerumani Der Klassiker itapigwa leo kati ya vigogo wa soka la Ujerumani Borussia Dortmund wakiwa nyumbani dhidi ya mabingwa mara nyingi wa Bundesliga Bayern Munich.
Mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Signal Iduna Park saa moja na nusu usiku utawakutanisha makocha wapya kwenye dabi hiyo Vicent Kompany wa Bayern Munich na Nuri Sahin aliyeanza majukumu ya kuifundisha Dortmund kama kocha mkuu june mwaka huu.
The bavarian Bayern Munich wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa ndio vinara wa Bundesliga baada ya kucheza michezo 11 na kukusanya alama 29 na hawajapoteza mchezo hata mmoja.
Dortmund wako nafasi ya tano kwenye msimamo wa Bundesliga wakiwa wamekusanya alama 19 pekee huku na wamedondosha alama 3 kwenye michezo minne mpaka sasa.
Klabu hizo zimekutana mara 110 kwenye ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga huku Bayern akiwa ndiye mbabe wa Dortmund akipata ushindi mara 54 na Dortmund akipata ushindi mara 26 tu na michezo 30 ikitamatika kwa sare.
Nani kuibuka mbabe leo ?