Kivumbi leo...! Siku ya burudani ndani na nje ya uwanja.
Joyce Shedrack
June 15, 2024
Share :
Michuano ya EURO 2024, inaendelea kutimua vumbi leo hii Nchini Ujerumani mara baada ya mechi za ufunguzi siku ya jana mwenyeji akianza kwa kishindo kwa kumtandika Scotland 5-1.
Uhispania ambaye ni bingwa mara tatu wa michuano hiyo mara ya mwisho akichukua kombe hilo mwaka 2012,atashuka dimbani majira ya saa moja usiku kumenyana na Timu ya Taifa ya Croatia ambayo haijawahi kushinda taji hilo.
Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa juni 18,2023 kwenye mashindano ya UEFA Nations League mchezo uliotamatika kwa sare ya bila kufungana na kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.
Tofauti na burudani itakayopatikana ndani ya uwanja mchezo huo unatajwa kuwa miongioni mwa michezo itakayofatiliwa zaidi kutokana na uwepo wa mashabiki wa Timu ya Taifa ya Croatia waliojenga ushawishi wa kuwavutia watu wengi.
Michezo mingine itakayopigwa hii leo ni Italia vs Albania 04:00 usiku.
Na Hungary vs Uswizi saa 10:00 jioni.