pmbet

Kivumbi na jasho CCM Kirumba, Yanga dhidi ya Singida

Sisti Herman

April 14, 2024
Share :

Nyasi za dimba la CCM Kiruma leo zitashuhudia mchuano mkali wa mchezo wa ligi kuu kati ya klabu ya Singida Fountaon Gate watakaowakaribisha Wananchi klabu ya Yanga kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza kuanzia saa 10 kamili jioni.

Yanga wanakwenda kutafuta ushindi ili kuendelea kujisimika kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na kuongeza tofauti ya alama na wanaowafuatia kwani wakishinda watakuwa na alama 55, tofauti ya alama 8 na Azam wanaowafuatia, pia tofauti ya alama 9 na Simba ambao watakuwa na mchezo mmoja mkononi.

Singida wanahitaji kushinda mchezo huu ili kutoka kwenye nafasi za chini, kwani wakishinda watakuwa na alama 27na kupanda hadi nafasi 7 kwenye msimamo wa ligi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri kutoshuka daraja.

Je watatoka?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet