Kivumbi na Jasho leo, Brazil dhidi ya Hispania Santiago Bernabeu
Sisti Herman
March 26, 2024
Share :
Leo usiku nyasi za uwanja wa Santiago Bernabeu, nyumbani kwa Real Madrid zitachakazwa sana kwani mabingwa mara 5 wa kombe la Dunia timu ya Taifa Brazil watakuwa wageni wa timu ya Taifa Hispania kwenye mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA.
Brazil ambao wapo nafasi ya 5 kwenye viwango vya FIFA wametoka kuwafunga timu ya Taifa ya Uingereza 1-0 kwenye dimba la Wembley.
Hispania ambao wapo nafasi ya 8 kwenye viwango vya FIFA wametoka kuwafunga 1-0 timu ya Taifa ya Colombia.
Picha, ni nyota wanne wa timu hizo wanaocheza ligi kuu Hispania, utoka kulia kwao;
1. Lamine Yamal, Hispania - Barcelona
2. Vinicius Jr, Brazil - Real Madrid
3. Nico Williams, Hispania - Athlethic Club
4. Rodrigo, Real Madrid - Brazil