Kiwango kikubwa cha Dawa za kulevya kwenye historia ya Tanzania chakamatwa
Eric Buyanza
December 27, 2023
Share :
Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini kupitia operation kubwa imefanikiwa kukamata kiwango kikubwa cha Dawa za kulevya aina ya Methamphetamine ambacho hakijawahi kukakamatwa kwenye historia ya Tanzania.
Akiongea na wanahabari Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, Aretas James Lyimo, amesema kukamatwa kwa mtandao huo ni mafanikio makubwa, kwani kiwango hicho cha dawa (Kilo 3182) kama kingefanikiwa kuingia mtaani kingeweza kuathiri watu zaidi ya Milioni 70, idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya raia wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Kamishna mtandao huo umekuwa ukifunga dawa hizo kwenye vifungashio vya majani ya chai na kahawa na hivyo kuwa ngumu kugundulika.
Mapapa 7 wa biashara hiyo ya madawa ya kulevya wamekamatwa, miongoni mwao wakiwemo wenye asili ya Asia na raia wa Tanzania.