KIZAZI KIPYA ARGENTINA: Nico Paz kurithi uzi namba 10 wa Messi
Eric Buyanza
September 17, 2026
Share :

Kiungo mshambuliaji chipukizi wa klabu ya Como 1907 ya nchini Italia, Nico Paz, anatarajiwa kukabidhiwa rasmi jezi iconic namba 10 ya Timu ya Taifa ya Argentina. Hatua hii inakuja kama sehemu ya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi hicho kufuatia kustaafu kwa nahodha na mchezaji nguli, Lionel Messi, baada ya fainali za Kombe la Dunia za hivi karibuni.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Argentina, kocha mkuu wa timu hiyo, Lionel Scaloni, amemchagua kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 kuwa mrithi sahihi wa jezi hiyo yenye uzito mkubwa wa kihistoria.
Uamuzi wa kumkabidhi Paz jezi hiyo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango chake bora anachokionyesha sasa katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A), ambapo tayari anavaa jezi namba 10 kwenye klabu yake ya Como. Viongozi wa ufundi wa Argentina wanamtazama kama 'modern playmaker' mwenye uwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo, kupiga pasi za mwisho, na kufunga.
Je, ataweza kufuata nyayo za Messi na kuandika historia yake mwenyewe?





