KIZUNGUMKUTI: Trump atangaza vita ya kuitenga kabisa Iran kiuchumi
Eric Buyanza
August 20, 2026
Share :

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kile alichokiita "operesheni kali zaidi ya kiuchumi kuwahi kuchukuliwa dhidi ya nchi yoyote ile" kwa lengo la kuitenga kabisa Iran kiuchumi duniani. Tangazo hili ametoa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social baada ya nchi hizo mbili kushindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mzozo unaoendelea.
Trump amesema itakuwa "vita vya kiuchumi na kubaguliwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa".
Hatua hizo zinajumuisha kuzuia kabisa magendo ya mafuta, mifumo ya kubadilishana fedha, uhamishaji wa fedha taslimu, na kampuni zinazotumika kuficha biashara za Iran.
Vikwazo hivi ni mwendelezo wa kampeni kubwa ya shinikizo inayoratibiwa na Wizara ya Fedha ya Marekani chini ya jina la 'Operation Economic Fury'





