Klabu ya Simba kuanza rasmi kutoa kadi ya uwanachama tarehe 27 March.
Joyce Shedrack
February 10, 2026
Share :
Klabu ya Simba imetangaza rasmi kuwa itaanza kutoa kadi za uwanachama kwa mashabiki wa timu yao kuanzia tarehe 27 mwezi wa tatu na kadi hizo zitakuwa kwenye mfumo wa kisasa.
“Leo tumekusanyika hapa kwa jambo la muda mrefu ambalo limesubiriwa sana. Tulikuwa tunatafuta kampuni ya uhakika kutengeneza kadi za Simba, kadi ambazo zinafanana na timu kubwa kabisa Afrika.”
“Bodi ya Wakurugenzi inapenda kuitangaza kampuni ya Mainstream kuwa ndio itatengeneza kadi za mfumo wa kileo na za kisasa na imeichagua kampuni ya Nexus kutoa kadi hizi za wanachama. Kadi hizi zitakuwa aina ya VISA.”
“Hii inakwenda kuwa Visa card pamoja na kukutambua kwamba ni mwanachama wa Simba lakini pia unaweza kuweka pesa, ukafanya malipo na miamala.”- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori.





