Klopp aagwa Liverpool, amtaja mrithi wake
Sisti Herman
May 20, 2024
Share :
Baada ya jana kushinda 2-0 dhidi ya Wolves kwenye mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu Uingereza msimu huu, klabu ya Liverpool jana imetumia wasaa huo kumuaga kocha wao mkuu Jurgen Klopp kwenye dimba la Anfield baada ya kutangaza mapema mwaka huu kuwa huu utakuwa msimu wake wa mwisho.
Klopp wakati wa hotuba yake pia alithibitisha kocha mkuu ajaye wa klabu hiyo kwakuanzisha nyimbo inayotaja jina la kocha wa Feyenoord ya Uholanzi Arne Slot.
Klopp anaondoka Liverpool kama shujaa baada ya kutwaa mataji 7 ikiwemo;
- Uefa Champions League
- Kombe la dunia la vilabu
- Uefa Super Cup
- Ligi kuu Uingereza
- Kombe la FA
- Kombe la ligi (Carabao) mara 2
- Ngao ya jamii