pmbet

Klopp afichua jinsi Liverpool ilivyoshindwa kumsajili Mbappe

Eric Buyanza

July 10, 2026
Share :

Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amefichua kuwa klabu hiyo ilifanya kila juhudi kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa, Kylian Mbappe, kujiunga na kikosi hicho mwaka 2017, lakini jitihada hizo hazikufanikiwa.

 

Klopp amesema Liverpool iliandaa ndege binafsi pamoja na huduma maalumu za chakula kwa Mbappe na familia yake ili kuwavutia kuhamia Anfield, wakati nyota huyo alipokuwa na umri wa miaka 18 akiichezea Monaco.

 

Klopp alisema huo ulikuwa "usajili ghali zaidi ambao haukukamilika" kwa Liverpool kutokana na rasilimali zilizowekezwa katika kumshawishi mchezaji huyo.

Mbappe aliamua kujiunga na Paris Saint-Germain (PSG) badala ya Liverpool mwaka 2017, kabla ya baadaye kuhamia Real Madrid, ambako anaendelea na maisha yake ya soka.

 

Kauli ya Klopp imeibua upya mjadala kuhusu namna Liverpool ilivyokuwa karibu kumpata mmoja wa wachezaji bora duniani, lakini ikashindwa kukamilisha dili hilo muhimu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet