Klopp afunguka ugomvi na Salah "Tumeyamaliza", Salah agoma kuongea
Sisti Herman
April 28, 2024
Share :
Kwenye sare ya 2-2 dhidi ya West Ham kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza kulitokea sintofahamu akwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp na mshambuliaji wake Mohammed Salah walionekana wakizozana kabla ya Mchezaji huyo kuingia uwanjani akitokea benchi.
Baada ya mchezo Klopp amesema sio sawa kulizungumzia hilo kwa sasa na kwa upande wake amemalizana nalo kwenye vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo.
“Siwezi kuongea kwa sasa , tayari tumeongea kwenye dressing room kwa upande wangu limeisha”
Hata hivyo Sallah aligoma kuongelea tukio hilo alipoombwa na waandishi wa habari akidai ataleta mtafaruku zaidi.