pmbet

Klopp alia na majeraha Liver

Sisti Herman

February 22, 2024
Share :

Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp ametoa taarifa ya ongezeko la majeruhi kwenye kikosi chake baada ya taarifa ya jeraha la goti la mshambuliaji wake Diogo Jota aliyotoa mara baada ya mchezo wa ligi kuu Uingereza jana dhidi ya Luton town ambapo walishinda 4-1.

 

"Diogo Jota ana tatizo la goti, itamchukua zaidi ya mwezi mmoja kumpata tena, Alisson anakabiliana na jeraha la misuli, kwa hivyo ameondolewa, Curtis Jones mwenye tatizo la kano ya mfupa, ameondolewa, Trent Alexander-Arnold yuko njiani kurudi lakini bado, Szoboszlai bado hajawa tayari, bado hajafanya mazoezi ya timu" alisema Klopp.

 

Ongezeko hilo la majeraha linafanya Liverpool ambao wapo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Uingereza kuwa na majeruhi zaidi ya 10 baada ya Matip, Badjcetic, Szoboszlai, Thiago, Trent, Jones, Nunez, Allison na Salah.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet