Klopp anaandaa kizazi kipya Ujerumani
Sisti Herman
September 16, 2026
Share :

Kocha mpya wa Ujerumani Jurgen Klopp aliahidi kuleta mapinduzi katika timu ya taifa ya Ujerumani na ametimiza ahadi hiyo kwa kuwaita wachezaji watatu kutoka timu ya taifa ya vijana ikiwa ni sehemu ya kutengeneza kizazi kipya cha soka la taifa hilo.
Said El Mala, Tom Bischof na Kevin Schade wote wanatarajiwa kuitwa kwenye kikosi kipya huku wachambuzi wengi wakisema ni wakati mwafaka kwa kizazi kijacho kupata fursa ya kuitumikia nchi yao.





