Klopp apoteza pete yake ya ndoa akishangilia
Sisti Herman
January 2, 2024
Share :
Kocha wa Liverpool Fc Jurgen Klopp jana wakati akishangilia ushindi wa 4-2 dhidi ya Newcastle United alinaswa na Camera za warusha matangazo wa Sky Sports akitafuta pete yake ya ndoa aliyoiangusha wakati akishangilia kwa furaha.
Hata hivyo baada ya muda alifanikiwa kuipata kwa msaada wa video za warusha matangazo baada ya kumuomba mmoja wa waongozaji wa chumba cha kuchanganya picha za video.