pmbet

Klopp kuondoka mikono mitupu Liverpool

Sisti Herman

April 25, 2024
Share :

Baada ya jana kuchezea kichapo cha 2-0 kutoka kwa watani zao Everton kwenye 'Merseyside Derby' kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 97 kwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp kuondoka mikono mitupu mwishoni mwa msimu.

Licha ya kubeba taji la EFL au Carabai Cup, lakini halitajwi kuwa moja kati ya makombe makubwa yanayokamilisha utatu wa mataji makubwa uitwao 'Treble' ambayo hujumisha Kombe lolote la Ulaya (Uefa CL, Europa), kombe la FA na ligi ya ndani ambapo mpaka sasa Liverpool wamebaki kwenye mbio za taji la ligi kuu ya Uingereza tu ambapo nako wana asilimia 3 tu za kutwaa baada ya kupeteza jana.

Liverpool wapo nafasi ya 2 kwenye msimamo wa ligi hiyo uliofikisha michezo 32 wakiwa na alama 74, Manchester City wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 73 huku wakiwa na michezo miwili ya akiba huku Arsenal wakiwa kileleni na alama 77. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet