Klopp kuwa kocha timu ya Taifa Marekani
Sisti Herman
July 11, 2024
Share :
Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp anahusishwa kuwa kwenye mahitaji ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa Marekani baada ya kuwa na kiwango duni chini ya kocha Gregg Berhalter.
Timu ya Taifa ya Marekani iliondolewa mapema kwenye hatua ya makundi ya kombe la Mataifa Amerika (Copa-Amerika) baada ya kushina nafasi ya 3 kwenye kundi C lililokuwa na timu za Uruguay, Panama na Bolivia.
Klopp ambaye aliondoka Liverpool baada ya msimu kutamatika alibainisha mapema mwaka huu kuwa atachukua likizo ya mwaka mzima kabla ya kurejea uwanjani.