KMC Yamtimua rasmi Marcio Maximo.
Joyce Shedrack
December 6, 2025
Share :
Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabaya, timu ya KMC imeamua kulivunja benchi lao la ufundi lililokuwa chini ya kocha Mbrazil Marcio Maximo.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni ilikuwa katika kipindi kigumu na kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars na Yanga SC.
Taarifa ya KMC inafafanua kuwa “ Tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Kocha Maximo pamoja na benchi lake la ufundi.
Tunatambua na kuthamini jitihada walizofanya katika kuboresha utendaji wa timu, ndani na nje ya uwanja, kwa ngazi ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla.
Hata hivyo, mabadiliko hayo hayakuweza kuleta matokeo ya haraka, kwani yanahitaji muda wa kutosha ili kuzaa matokeo yanayotarajiwa.
Tunamtakia Kocha Maximo na timu yake kila la heri na tunabaki wazi kuwatumia tena pindi fursa itakapojitokeza siku za usoni” ilisema taarifa ya timu hiyo.





