KMC Yavunja benchi lake la ufundi kisa matokeo mabovu.
Joyce Shedrack
April 4, 2026
Share :
Mfululizo wa matokeo mabaya inayoipata timu ya KMC katika kinyang’anyiro cha Ligi Kuu Bara kimefanya timu hiyo kulivunja benchi lake la ufundi.
Benchi hilo lililokuwa chini ya kocha Abdallah Mohamed ‘Baresi’ limevunjwa baada ya kipigo cha mabao 3-2 iliyokipata kikosi hicho kutoka kwa Mbeya City.
Taarifa iliyotolewa na Klabu ya KMC imesema kuwa wamekaa na kukubaliana pande zote na kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha huyo pamoja na benchi lake la ufundi.
“Tunatambua na kuthamini jitihada walizofanya katika kuboresha utendaji wa timu, ndani na nje ya uwanja, kwa ngazi ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla. Tunamtakia Kocha Bares na wasaidizi kila la kheri”
Taarifa ya timu hiyo imetolewa na
Ofisa Mtendaji mkuu wa kikosi hicho cha Kinondoni, Daniel
Madenyeka.





