pmbet

Kobbie, dogo aliyeiokoa Man Utd Jioooni

Sisti Herman

February 2, 2024
Share :

Kinda wa klabu ya Man Utd Kobbie Mainoo ambaye aliiokoa timu hiyo kwa goli lake la dakika za mwisho jana kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Wolves ambapo United walishinda kwa goli 4-3, amesema ametimiza ndoto alizoota akiwa mtoto.

 

“Siwezi kuelezea hizi hisia kiukweli, ndoto zangu zimekuwa kweli kwa klabu yangu ya toka utotoni kwenye mchezo mgumu kama huu wa ugenini dhidi ya timu ngumu kwa ushindi wa aina hii inavutia sana” alisema kinda huyo anayetumikia nafasi ya kiungo mithili ya Paul Pogba.

 

Kobbie amefunga mara ya pili mfululizo ndani ya siku 4 kwenye mashindano tofauti mara baada ya wikiendi iliyopita kufunga goli lake la kwanza akiwa na timu ya wakubwa ya United kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Newport.

 

Kwenye mchezo huo wa jana magoli ya United yalifungwa na Rashford, Højlund, McTominay na Mainoo ambaye alifunga dakika za usiku huku magoli ya magoli ya Wolves yakifungwa na Sarabia(Pen), Kilman na Neto aliyefunga dakika 2 kabla ya Kobbie kufunga la ushindi kabla ya mchezo kuisha.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet