pmbet

"Kobbie ni kama Yaya Toure" - Kocha

Sisti Herman

February 29, 2024
Share :

Kocha wa timu ya vijana wa Manchester United na aliyekuwa mchezaji wa Totenham Hotspurs Tom Huddlestone amesema siku ya kwanza mazoezi alivyomuona kiungo kinda wa klabu hiyo Kobbie Mainoo alimfananisha moja kwa moja na aliyekuwa kiungo wa Barcelona, Manchester City na timu ya Taifa ya Ivory Coast Yaya Toure kutokana na aina yake ya uchezaji.

 

"Katika siku yangu ya kwanza huko Carrington, nilikuja na kuwatazama vijana katika mafunzo, nilikuwa nikizungumza na rafiki yangu njiani kurudi nyumbani na kusema, Kuna vijana wawili ambao nimewaona mmoja wao ni mchezaji anayeitwa Kobbie Mainoo. Anaonekana kama Yaya Toure mpya...”

 

Kobbie aliyepandishwa kutoka timu ya vijana ya Man Utd hadi sasa amecheza na kufunga mabao kwenye michezo kadhaa ya ligi huku akitishia na kuwapa ushindani wa namba viungo wa daraja kubwa kama Casemiro na Sofiane Amrabat.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet