Kobe Mainoo kuongezewa mshahara mara 4, kulpwa Milioni 265 kwa wiki
Eric Buyanza
June 1, 2024
Share :
Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, mwenye umri wa miaka 19, anatarajiwa kumwaga wino kwenye mkataba wake mpya na Manchester United miezi michache ijayo...mkataba ambao klabu hiyo inatazamiwa kumuongezea mshahara mara nne ya mshahara wake wa sasa.
Mchezaji huyo tayari amefanya mazungumzo ya awali na klabu hiyo lakini atakuwa tayari kuweka wazi kuhusu mkataba wake mpya atakaporejea kutoka kwenye michuano ya Ulaya.
Mainoo amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza kwa Manchester United msimu huu.
Mchezaji huyo atalipwa takriban pauni 80,000 (sawa na shilingi milioni 265 za kitanzania) kwa wiki kwenye mkataba mpya.
Mainoo ameitwa katika kikosi cha muda cha England kwa ajili ya michuano ya Euro.