Kocha AC Milan kuungana na Benzema na Kante Saudia
Sisti Herman
July 3, 2024
Share :
Baada ya kufutwa kazi kama kocha mkuu ya AC Milan, mkufunzi, Stefano Pioli ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia akichukua mikoba ya Muargentina, Marcelo Gallardo.
Licha ya kusheheni nyota kama Karim Benzema, N’Golo Kante na Fabinho klabu hiyo ya Saudi Pro League ilikuwa na msimu usioridhisha ikimaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Pioli (58) raia wa Italia aliiongoza AC Milan kuanzia Oktoba 2019 mpaka mwisho wa msimu uliopita akiiongoza Milan kushinda Ligi Kuu Italia mnamo 2022 na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2022/23.