Kocha afungiwa Ujerumani kwa kumsukuma Sane
Sisti Herman
January 26, 2024
Share :
Chama cha Soka nchini Ujerumani, kimemfungia kocha wa Union Berlin, Nenad Bjelica mechi (3) na kupigwa faini ya Euro 25,000 kwa tukio ambalo lililoonekana akimsukuma winga wa Bayern Munich, Leroy Sane wakati wa mchezo wao January 24.
Kocha huyo aliijngia katika mzozo na kiasi cha kuoneshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo katika dakika ya 74, baada ya kumsukuma winga wa Bayern Munich, Leroy Sane, Mchezo ulimalizika kwa Bayern Munich kushinda goli 1-0.