Kocha aliyehusishwa kutua Simba atambulishwa Mamelodi.
Joyce Shedrack
July 6, 2024
Share :
Klabu ya Mamelodi Sundowns imetangaza kumrejesha kwenye timu kocha wao wa zamani Steve Komphela kuwa mkufunzi wao akirithi mikoba ya Rhulani Mokwena waliyetangaza kuachana naye siku chache zilizopita.
Komphela ambaye alishawahi kukinoa kikosi cha masandawana alikuwa ni miongoni mwa makocha waliotajwa kuhitajika na wekundu wa msimbazi Simba kabla ya jana klabu hiyo kumtambulisha Davis Faldu kama kocha Mkuu wa timu hiyo.
Mamelodi Sundowns tayari imeanza mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao nchini Afrika Kusini na siku chache zijazo wataondoka Nchini humo kuelekea Austria watakapoweka kambi ya maandalizi (Pre season).