Kocha amfuata Feitoto Azam
Sisti Herman
January 15, 2024
Share :
Kocha Mohamed Salah ‘Rijkaard’ ambaye alikiibua na kukikuza kipaji cha Feisal Salum ‘Feitoto’ amevutwa Azam FC kuhudumu kwenye timu za vijana.
Rijkaard alianza kumfundisha Feitoto tangu akiwa kijana mdogo na kuendelea kuwa nyuma ya mchezaji huyo akiwa JKU, Yanga na sasa Azam FC.
Wawili hao [Kocha Rijkaard na Feitoto] wanaungana tena pale Chamazi wakiwa waajiriwa, Rijkaard Kocha wa timu za vijana za Azam FC na Feitoto ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Azam FC.
Kocha Rijkaard alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 15 ya Zanzibar [Karume Boys] ambayo ilishinda ubingwa wa CECAFA U15 Boys Championship 2023 mwezi Novemba 2023 nchini Uganda.