Kocha Edin Terzic aibwaga Dortmund
Joyce Shedrack
June 13, 2024
Share :
Kocha Mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Edin Terzic amejiuzulu nafasi yake klabuni hapo baada ya kuiandikia klabu hiyo barua ya kutaka kuachia ngazi hiyo ikiwa ni wiki mbili tu tangu aiongoze timu hiyo kucheza Fainal ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Terzic tangu ajiunge na Dortmund mwaka 2022 ameisaidia timu hiyo kushinda kombe moja pekee la DFB Cup huku akisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya 2 kwenye ligi kuu ya Ujerumani mwaka 2023.
Dortmund msimu huu kwenye ligi kuu ya Ujerumani imemaliza nafasi ya 5 nyuma ya Rb Leipzig, Bayern Munich, VFB Stuttgart na Bayer Liverkusen waliokuwa mabingwa wa Ligi hiyo.
Akiwaaga mashabiki wa Dortmund Terzic amesema “Ingawa inauma sana, nataka kuwajulisha kwamba ninaondoka BVB leo. Ilikuwa heshima kubwa kuiongoza klabu hii hadi fainali ya Kombe la DFB na hivi majuzi fainali ya Ligi ya Mabingwa,” Terzic.