Kocha Man Utd anukia Bayern
Sisti Herman
May 1, 2024
Share :
Rais wa klabu ya Bayern Munich Harbert Hainer amethibitisha kuwa klabu hiyo ipo kwenye hatua nzui za mazungumzo na aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United Ralph Rangnic kwaajili ya kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo yenye mataji mengi zaidi Ujerumani.
Rangnic ambaye kwasasa ni kocha wa timu ya Taifa ya Austria, anasifika kwa kuweza kuongoza miradi endelevu ya kiufundi kama kuwa kocha mkuu, Mkufunzi wa makocha au Mkurugenzi wa Ufundi.
Kocha huyo Mjerumani pia anasifika kwa falsafa za soka la asili ya Ujerumani na pia alishawahi kuwanoa kwa nyakati tofauti makocha wakubwa wa Ujerumani kama Thomas Tuchel wa Bayern, Jurgen Klopp wa Liverpool na Juilien Negelsman wa Ujerumani.