Kocha Mashujaa abwaga manyanga
Eric Buyanza
December 9, 2023
Share :
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya klabu ya Mashujaa ya kigoma zimeeleza kuwa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali kuhusu kujiuzulu kwa Kocha mkuu wa timu hiyo Abdallah Mohamed 'Baresi' ikiwa ni saa chache baada ya kufumuliwa nyumbani mabao 2-0 na Tanzania Prisons ni za kweli.
Baresi amefikia uamuzi wa kuandika barua ya kujiuzulu baada ya matokeo yasiyoridhidhisha kwenye mechi nane mfululizo bila kupata ushindi katika Ligi Kuu Bara.
Mara ya mwisho kwa Mashujaa kushinda mechi ya ligi ilikuwa Septemba 16 ilipoifumua Ihefu kwa mabao 2-0 mjini Kigoma, lakini baada ya hapo ni mechi mbili tu ilizovuna pointi kwa kutoka sare, huku sita nyingine ikipoteza na kuifanya timu hiyo iteme jumla ya 22 katika mechi nane zilizopita.