Kocha mkuu wa Nigeria apata wakala mpya
Eric Buyanza
February 19, 2026
Share :
Kocha mkuu wa Super Eagles, Eric Chelle amesaini mkataba na wakala mpya wa usimamizi.
Hivi majuzi Chelle alisitisha uhusiano wake na wakala Abraham Sidibe, ambaye alifanikisha uteuzi wake kama kocha mkuu wa timu ya taifa (Super Eagles).
Raia huyo wa Mali alijiongezea hadhi baada ya kuiongoza Super Eagles hadi nafasi ya tatu kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika la 2025 nchini Morocco.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa Super Eagles mnamo Januari 2025 kwa mkataba wa miaka miwili.
Chelle alihusishwa na nchi kadhaa barani Afrika baada ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, na pia amehusishwa na klabu ya Olympic Marseille.






