pmbet

Kocha Morocco aihofia Taifa Stars

Sisti Herman

January 17, 2024
Share :

Kocha mkuu wa kikosi cha Morocco Walid Regragui ameweka wazi kuwa kesho wataingia na tahadhari kubwa kuikabili Tanzania huku wakiiheshimu kutokana na matokeo ambayo timu zingine zimepata kwenye timu zenye hadhi ya Tanzania.

 

“Tutaingia Uwanjani Kesho huku tukiiheshimu Tanzania, tumeshuhudia katika Michezo ya awali kwa wenzetu wakisumbuliwa na Timu zenye hadhi kama ya Tanzania na hii inaizidi kudhihirisha kwamba Mashindano haya ni Magumu Msimu huu”.

 

“Tunatakiwa kupambana kwasababu kila mmoja anataka kuweka historia yake”, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Morocco, Walid Regragui.

Taifa Stars itashuka dimbani kesho kuikabili timu ya Taifa ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa kundi F wa fainali za matifa ya Afrika [AFCON] zinazoendelea nchini Ivory Coast.

 

Hadi kufikia hivi sasa mataifa yaliyokuwa yanapewa uzito wa kufanya vizuri kalingana na mpinzani kwenye michezo yake ya mwanzo yameshindwa kufua dafu.

 

Hii ni karata mhimu kwa Taifa Stars na Adel Amrouche hapo kesho kuusaka ushindi kwa mara ya kwanza mbele ya Morocco tangu michuano hii ianzishwe ikiwa Tanzania imeshiriki mara tatu na haijawahi kupata ushindi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet