pmbet

Kocha mpya wa kumnoa Selemani Mwalimu anatoka Ureno.

Joyce Shedrack

July 27, 2026
Share :

Klabu ya Wydad Athletic ya Morocco imemtangaza rasmi Paulo Sérgio kuwa kocha wake mpya kuelekea msimu wa 2026/27.

 

Kocha huyo raia wa Ureno amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza muda endapo pande zote mbili zitaridhishwa na mwenendo wa timu.

 

Uongozi wa Wydad unaamini ujio wa Paulo Sérgio utafungua ukurasa mpya kwa klabu hiyo, ambayo inalenga kurejea katika ushindani mkubwa wa soka la Morocco na mashindano ya kimataifa.

 

Paulo Sérgio anajiunga na Wydad akiwa na uzoefu wa kuzinoa klabu mbalimbali barani Ulaya na Asia, huku akipewa jukumu la kuijenga upya timu na kuirejesha kwenye mafanikio katika msimu ujao.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet