Kocha Mwanamke aweka rekodi kufundisha timu ya wanaume Ujerumani
Sisti Herman
June 19, 2024
Share :
Akiwa na umri wa miaka 32 tu, Mrembo Sabrina Wittmann raia wa Ujerumani, ameandika historia barani Ulaya baada ya kuteuliwa kuwa kocha Mkuu wa kwanza mwanamke kufundisha timu ya wanaume ya madaraja ya juu ua ushindani baada ya kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa FC Ingolstadt 04 ya ligi daraja la pili nchini humo.
Kabla ya kuwa kocha Sabrina alipata kuwa kiungo mshambuliaji wa timu ya Wanawake ya klabu hiyo kisha akaamua kujiongeza kusoma kozi za ukocha na baadae kuibukia kwenye ukocha.
Nchini Tanzania, Fatuma Omary kipa wa zamani wa Twiga Stars na Edna Lema 'Mourinho' wanashikilia rekodi ya kuwa makocha wa mwanzo kabisa kunoa timu za wanaume, Fatuma alikuwa kocha wa makipa wa KMC na Edna ni kocha msaidizi wa Biashara United ya mara.