pmbet

Kocha Senegal apona baada ya kuugua ghafla Afcon

Sisti Herman

January 22, 2024
Share :

Kocha wa timu ya taifa ya Senegal, Aliou Cisse alipata matatizo ya kiafya, akawahishwa hospitali ya mjini Yamoussoukro ambako alilazwa usiku mzima baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi Cameroon, lakini sasa anaendelea vyema baada ya matibabu. 

 

Taarifa ya shirikisho la soka la Senegal kupitia kwa msemaji wa timu ya Senegal, Kara Thioune, ilisema: “Vipimo alivyofanyiwa vimemhakikishia yuko sawa na amerejea kundini. Anaendelea vyema,” ilibainisha sehemu ya taarifa kuhusu Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea kikosini kwake.

 

Simba wa Teranga waliendeleza mwanzo mzuri wa kutetea taji lao la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1 na kutinga kibabe hatua ya 16 Bora.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet