Kocha Simba ajiunga na Dynamos
Sisti Herman
March 28, 2024
Share :
Aliyewahi kuwa kocha wa klabu ya Simba Patrick Phiri ameteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa michezo wa klabu ya Kansanshi Dynamos ya nchini Zambia.
Kocha huyo Mzambia anashikilia rekodi ya kuisaidia Simba kutwaa taji la ligi kuu Tanzania bara bila kufungwa (UNBEATEN) msimu wa 2010/13.