pmbet

Kocha Simba ateuliwa Uganda, adai bado anaipenda Simba

Sisti Herman

December 28, 2023
Share :

Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba Queens ambaye kwasasa ni kocha wa timu ya Taifa wanawake Uganda Charles Ayiekoh Lukula ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Kampala Queens ya ligi kuu wanawake nchini Uganda.

 

“Nashukuru uongozi wa Kampala Queens kunipa nafasi hii, tumekuja Kampala tukijua ni mabingwa, tumepewa malengo matatu, kutetea ubingwa ligi, tufuzu CECAFA na kuendeleza vijana” alisema Lukula akiongea na mkuu wa idara ya habari ya timu hiyo Hassan Mulongo.

 

"Mimi ni shabiki wa Simba, naipenda Simba, ni timu yangu namba moja Afrika Mashariki, wasalimie Watanzania, Nguvu Moja” alisisitiza Lukula alipotafutwa na PM Sports .

 

Ayekoh aliyeifikisha Simba nusu fainali ya ligi ya mabingwa wanawake msimu wa 2022/23 alidumu msimbazi kwa msimu mmoja pekee kabla ya kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya Taifa Uganda huku mikoba yake Simba ikichukuliwa na Juma Mgunda na Mussa Mgosi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet