Kocha Stras kutangaza jeshi la mwisho AFCON leo
Sisti Herman
January 1, 2024
Share :
Leo Jumatatu, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Adel Amrouche anatarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji 27 ambao watakwenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya AFCON inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni nchini Ivory Coast.
Hapo awali kocha huyo alitangaza kikosi cha wachezaji 50 ambapo tayari aameshakata majina 23 na kubakiwa na wachezaji 27 ambapo leo January 1 kocha huyo atatangaza kikosi cha wachezaji hao 27.
Tayari baadhi ya mataifa Yalishatangaza vikosi vyao na Mataifa Mengine tayari yameshaingia kambini,kama Wenyeji Ivory Caost, Zambia, Mali, Senegal, Misri na Cameroon.