pmbet

Kocha Tabora kuondoka

Sisti Herman

March 20, 2024
Share :

Mara baada ya matokeo mabaya mfululizo kwa klabu ya Tabora United ligi kuu Tanzania bara, taarifa za ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kocha wao Goran Kapunovic kuachana na timu hiyo huku ikidaiwa kutoridhishwa na baadhi ya mambo kwenye uongozi.

 

"Taarifa zilizopo mwalimu tunaweza tusiwe naye japo haziko moja kwa moja" neno la Kocha Msaidizi wa Tabora United, Bernard Fabian kuhusiana na suala kuondoka Kocha Goran Kopunović na muendelezo wa matokeo yasiyoridhisha kwenye NBC Premier League (Azam Tv).

 

“Linapokuja swala la kocha kutuaga hakuna atakayependa, tutaumia”  nukuu ya nahodha wa Kikosi hicho, Said Mbathy kuhusiana na suala kuondoka Kocha Goran Kopunović (Azam Tv)

 

Hadi sasa Tabora United ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi huku ikiwa na mwendelezo usioridhisha kwani kwenye michezo mitano iliyopita wakiwa wamepoteza michezo mitatu na kushinda mmoja.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet