Kocha wa Atletico Madrid EL Cholo awanyooshea mikono Barcelona.
Joyce Shedrack
September 21, 2026
Share :
Kocha wa Atlético Madrid, Diego Simeone, ametoa kauli za heshima kuhusu klabu ya Barcelona akieleza kuvutiwa na kiwango cha timu hiyo kwa sasa.
Akizungumza na ESPN, Simeone amesema Barcelona wanaonekana kucheza katika kiwango tofauti na timu nyingine.
“Inaonekana Barcelona wanacheza mchezo tofauti na ule tunaoucheza sisi. Hawakuwa na mshambuliaji namba 9 wa kawaida, kisha Raphinha akaibuka na kufunga mabao 12 hadi sasa ni jambo la kushangaza.”
Simeone pia amemsifu nyota wa Barcelona, Lamine Yamal, ambaye tayari amefunga mabao saba, huku akieleza namna Barcelona wanavyowasumbua wapinzani kwa presha yao kubwa.
“Lamine Yamal amefunga saba. Wanakushinikiza hata kwenye uwanja wako na kukunyima muda wa kufanya maamuzi. Hawaogopi kuchukua hatari, wala hawaogopi kufungwa bao wanaonekana kuwa kwenye kiwango kingine.”
Kocha huyo wa Atlético ameongeza kuwa Barcelona wana uwezo wa kutumia hata kufungwa kama motisha ya kuimarika zaidi.
“Inaonekana namna wanavyopokea bao dhidi yao huwafanya wawe bora zaidi. Mimi binafsi, naichukulia Barcelona kuwa timu bora zaidi kwa sasa.” kocha wa Atletico El Cholo.





